Loading...

WAKAZI WALINDI WAJIKUSANYA UWANJA WA ILULU KUADHIMISHA 'SIKU YA UTEPE MWEUPE'

Loading...
Wakazi wa mkoani Lindi wamekusanyika katika uwanja wa mpira wa Ilulu kuadhimisha 'Siku ya Utepe Mweupe'.

Utepe mweupe ni kampeni maalum ya kukuza afya bora kwa wakina mama na kuwawezesha kuwapatia huduma stahiki za kiafya.

Tukio hili limeanza mapema ya leo kwa maandamano kutoka Uwanja wa Fisi mpaka Ilulu.

Maandamano hayo ambayo yaliyohusisha wakazi, wafanyakazi kutoka serikalini na mashirika mbali mbali yasiyo ya kiserikali yaliongozwa na polisi na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw Godfrey Zambi.

Bw Zambi alipitia mahema yote ya maonesho yaliyoelezea shughuli mbali mbali wanazozifanya ikiwa ni pamoja na mpango wa uzazi, kujifungua salama kwa wamama na huduma zingine za afya zinazohusiana na wanawake.

Ushirika wa Utepe Mweupe ambao uliandaa tukio hilo wamewahamasisha mabaraza ya serikali za mitaa kutenga angalau asilimia 10 ya mapato yao ili kuhudumia mpango wa wakina mama kujifungua salama.
Na Shabani Rahis - Lindi

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Kitaifa punde zinapojiri.
WAKAZI WALINDI WAJIKUSANYA UWANJA WA ILULU KUADHIMISHA 'SIKU YA UTEPE MWEUPE' WAKAZI WALINDI WAJIKUSANYA UWANJA WA ILULU KUADHIMISHA 'SIKU YA UTEPE MWEUPE' Reviewed by By News Reporter on 3/16/2018 10:23:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.