Loading...

ZARI WA DIAMOND ANAZIDI KUPASUA ANGA LA MAFANIKIO LICHA YA KUACHANA BABA WATOTO WAKE

Loading...
Aliyekuwa mpenzi wa mwimbaji Diamond Platinumz, Zari Hassan amezidi kujichukulia umaarufu na kutengeneza mkwanja baada kusaini mkataba wa kibiashara na kampuni ya Kedz hapa nchini.

Wiki kadhaa kupita toka itangazwe kuwa ameachana na Diamond, kwa mara ya kwanza amerudi nchini kusaini mkataba na kampuni ya Diapers Manufacturing Company Kedz Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam siku ya Jumatano Zari a.k.a the Bosslady ambaye amebahatika kupata watoto wawili na Diamond - alisema dili hilo ni zuri kwa upande wake lakini hakuelezea kwa undani ni faida zipi atapata kutokana na mkataba huo wa kibiashara. Waandishi wa habari pia walikuwa na hamu ya kujua kinachoendelea katika mahusaino kwa sasa lakini alionekana kutopenda kuzungumzia swala hilo kwa sasa na kudai kilocho mleta hapa ni biashara tu na sio maisha yake ya kimahusiano kwa sasa.
Na Catherine Kisese.


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
ZARI WA DIAMOND ANAZIDI KUPASUA ANGA LA MAFANIKIO LICHA YA KUACHANA BABA WATOTO WAKE ZARI WA DIAMOND ANAZIDI KUPASUA ANGA LA MAFANIKIO LICHA YA KUACHANA BABA WATOTO WAKE Reviewed by By News Reporter on 3/29/2018 11:21:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.