Loading...

BODI YA FILAMU KENYA YAPIGA MARUFUKU FILAMU YA WAPENZI WA JINSIA MOJA

Loading...
Bodi la Filamu la Kenya (KFCB) imeipiga marufuku filamu iitwayo 'Rafiki' inayogusia masuala ya mapenzi ya jinsia moja.

Filamu hiyo ni ya kwanza kutoka Kenya kuchaguliwa ili kuonyeshwa katika tamasha la kimataifa la Cannes mwaka huu.

Tamasha la Cannes, ni miongoni mwa matamasha ya filamu makubwa duniani ikiwa pamoja na tamasha la Oscars. Wanafilamu,watayarishaji na waongozaji wa filamu wanakutana sio tu kushindanisha filamu lakini pia ni nafasi kubwa ya kuuza filamu zao kwa makampuni makubwa.

KFCB imepiga marufuku filamu hiyo kuonyeshwa hadharani au kutangazwa kwenye televisheni na kusambazwa, ikisema maudhui ya filamu hiyo inayoonesha mapenzi ya jinsia moja kati ya wanawake wawili, inakiuka sheria za Kenya.
Na Neema Joshua.




Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za burudani punde zinapojiri.
BODI YA FILAMU KENYA YAPIGA MARUFUKU FILAMU YA WAPENZI WA JINSIA MOJA BODI YA FILAMU KENYA YAPIGA MARUFUKU FILAMU YA WAPENZI WA JINSIA MOJA Reviewed by By News Reporter on 4/28/2018 11:48:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.