Loading...

MALAWI: JOYCE BANDA ARUDI NCHINI BAADA YA KASHFA YA UFISADI

Loading...
Rais wa zamani wa Malawi Joyce Banda amesema, hana wasiwasi wowote wa kukamatwa baada ya kurejea nyumbani wiki iliyopita.

Rais huyo wa zamani alikimblia nchi hiyo miaka minne iliyopita baada ya kuwepo kwa ripoti kuwa atakamatwa kwa madai ya ufisadi.

Akizungumza akiwa jijini Blantyre, Bi.Banda amesisitiza kuwa hajafanya kosa lolote na iwapo serekali inataka kumkamata basi ifanye hivyo.

Polisi wametoa kibali cha kukamatwa kwa rais Joyce Banda kufuatia tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na kutakatisha fedha.

Banda aliyekuwa Rais wa nchi hiyo tangu mwaka 2012 hadi 2014, aliondoka nchini humo Septemba 2014 ikiwa ni miezi michache kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu uliomweka madarakani Rais wa sasa, Peter Mutharika. Mpaka sasa Banda hajawahi kurudi tena nchini mwake.
Na Peter Godwin.




Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika punde zinapojiri.
MALAWI: JOYCE BANDA ARUDI NCHINI BAADA YA KASHFA YA UFISADI MALAWI: JOYCE BANDA ARUDI NCHINI BAADA YA KASHFA YA UFISADI Reviewed by By News Reporter on 4/30/2018 01:10:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.