Loading...

MASHABIKI WA LIVERPOOL KUADHIBIWA KWA KUSHAMBULIA BASI LA MAN CITY

Loading...
Ligi kuu ya UEFA imetangaza kuwa imeanzisha uchunguzi wa kina kuhusiana na shambulizi la mashabiki wa klabu ya Liverpool kwa wachezaji wa klabu ya Man City.

Imeripotiwa kuwa basi lililokuwa limewabeba wachezaji wa Man City lilishambuliwa na mashabiki wa Liverpool kwa kurushiwa chupa, vilipuzi na vijiti.

Sky Sports kupitia ukurasa wa Twitter zilidhibitisha kisa hicho na kutangaza kwamba huenda mashabiki wa Liverpool wakaadhibiwa vikali.

Aidha, Meneja wa klabu ya Liverpool Jurgen Kloppa aliomba msamaha kwa niaba ya timu hiyo kwa meneja wa Man City na kwa wachezaji wake kwa ujumla.

Kloppa alijutia kwa makaribisho hayo mabaya kwa wachezaji wa Man City na kuwaahidi kwamba ligi ya UEFA itawaadhibu vilivyo ili kitendo cha aina hiyo kisirudiwe tena.
Na Catherine Kisese
MASHABIKI WA LIVERPOOL KUADHIBIWA KWA KUSHAMBULIA BASI LA MAN CITY MASHABIKI WA LIVERPOOL KUADHIBIWA KWA KUSHAMBULIA BASI LA MAN CITY Reviewed by By News Reporter on 4/06/2018 04:25:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.