Loading...

MKE WA MKONGWE WA MUZIKI UGANDA CHAMELEON AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE

Loading...
Mwimbaji mkongwe nchini Uganda Joseph Mayanja, almaarufu Jose Chameleone na mke wake Daniela Atim wamepata mtoto.

Mtandao mmoja huko Uganda imeng’amua kuwa mke wa Chameleone alijifungua salama mtoto wa kike asubuhi ya Alhamisi, Machi 5, huko Marekani.

Chameleone na mke wake wamemwita binti yao Xara Amani Mayanja.

Habari kuhusu kuzaliwa kwa mtoto huyo kwanza zilitolewa na mwimbaji huyo wa kibao maarufu ‘Valu Valu’ Chameleone binafsi kupitia mtandao.

“Angalia alichonifanyia Mungu. Xara Amani Mayanja amejiunga nasi leo 7:14 am. Asante kwa Thanks Andreon Atim kwa uvumilivu wako, ukarimu wako, kunipenda na zaidi ya yote kunipa furaha yote mke anaweza mpa mumewe. Hongera kwa binti huyu mrembo. Karibu Xara Amani Mayanja. Asanteni kwa maombi yenu,” Chameleone ameandika katika picha ya mkewe akiwa na mtoto wao.
Huyu ni mtoto wa tano katika familia hii na wamekuwa wakiwalea watoto wao tangu miaka 10 iliyopita.

Maajuzi, mke wa Chameleon alizua mjadala mkubwa mtandaoni baada ya kuzianika picha zake za ‘utupu’ na ujauzito wake jambo ambalo wengi hawakulifurahia. Hata hivyo kuna waliofurahia picha hizo.
Na Catherine Kisese.


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
MKE WA MKONGWE WA MUZIKI UGANDA CHAMELEON AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE MKE WA MKONGWE WA MUZIKI UGANDA CHAMELEON AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE Reviewed by By News Reporter on 4/06/2018 01:59:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.