Loading...

MREMBO ALIYEFUNGIWA NA BASATA ATIMULIWA NA MWENYE NYUMBA WAKE

Loading...
BAADA ya kufungiwa kujishughulisha na sanaa ya filamu na muziki kwa miezi sita na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza kwa kuvaa nusu utupu, mwanadada Suzan Michael ‘Pretty Kind’ ameponzwa na waziri huyo kwani amekutwa na balaa lingine, Risasi Jumamosi linakupa habari kamili.

Habari za awali zilidai kwamba, Pretty kwa sasa yupo kwenye wakati mgumu kwani amefukuzwa katika nyumba aliyokuwa akiishi kisa mwenye nyumba hataki mpangaji anayevaa nusu utupu.

“Mambo ni magumu sana kwa Pretty kwani amepewa ‘notice’ kwenye nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya Sinza, sasa ndiyo anahaha kutafuta pa kuishi, kiukweli tangu amefungiwa amejikuta akipoteza dira kabisa,” alidai rafiki wa Pretty.

Gazeti moja hapa nchini Jumamosi lilimtafuta Pretty ili kujua ukweli ambapo alipopatikana alifunguka kwa kuthibitisha madai hayo na kueleza kuwa amepewa ‘notice’ ya kuhama kwenye nyumba aliyokuwa akiishi.

“Ukweli ni kwamba tangu nimefungiwa na naibu waziri nimekuwa nikinyanyasika sana, hapa baba mwenye nyumba kanifukuza na kwenye sehemu niliyokuwa nimelipia kwa ajili ya biashara nako amenifukuzwa, naumia kwa kweli maana nimeshabadilika lakini bado watu wananiona ni mvaa nusu utupu tu,” alisema Pretty na kukiri kuwa kwa sasa anahaha kutafuta nyumba ya kuishi.
Na Geofrey Okechi.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
MREMBO ALIYEFUNGIWA NA BASATA ATIMULIWA NA MWENYE NYUMBA WAKE MREMBO ALIYEFUNGIWA NA BASATA ATIMULIWA NA MWENYE NYUMBA WAKE Reviewed by By News Reporter on 4/14/2018 08:45:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.