Loading...

MSITU WA KAZIMZUMBWI KUREJESHWA HALI YAKE YA ZAMANI

Loading...
Muongo mmoja uliopita hifadhi ya msitu wa Kazimzimbwi uliopo wilaya ya Kisarawe, mkoa wa Pwani, Tanzania ulikuwa unaangamia kutokana  na shughuli hasi za binadamu na usimamizi mbovu wa mamlaka husika. Shughuli hizo za kibinadamu ni kama: Kuchoma Mkaa na ujenzi wa makazi ya binadamu.

Lakini leo, msitu huo unaoitwa "Mapafu ya Dar es Salaam" taratibu unaanza kurejesha hadhi yake ya awali, kutokana na juhudi za serikali pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Msitu kwa kipindi kirefu kuanzia miaka ya 1960, umekuwa ukisaidia upatikanaji wa mvua, kusafisha hewa mkaa inayotakana na viwanda na shughuli za kibinadamu na hata kuzuia baadhi ya maradhi ya mimea chakula.

Msitu huo ni kati ya misitu mikongwe duniani iliyosalia ulimwenguni ambao unavyanzo vya maji vingi. Serikali hii ya awamu ya tano imekusudia kupambana na waharibifu wa msitu huo ndio maana kwa sasa maeneo ya Pwani ya nchi zinapatikana mvua za kutosha kama ilivyokuwa hapo nyuma.
Na Geofrey Okechi.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mazingira punde zinapojiri.
MSITU WA KAZIMZUMBWI KUREJESHWA HALI YAKE YA ZAMANI MSITU WA KAZIMZUMBWI KUREJESHWA HALI YAKE YA ZAMANI Reviewed by By News Reporter on 4/14/2018 08:16:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.