Loading...

MTU MMOJA AAPA KUJIUA KISA MIGUNA MIGUNA - KENYA

Loading...
Mtu mmoja kutoka Kisumu amewaacha wengi kinywa wazi baada ya kuamua kusalia njaa kwa siku kadhaa kama hatua ya kuitaka serikali kumruhusu Miguna kuingia nchini Kenya.

Mtandao mmoja wa nchini Kenya ulibaini kuwa mtetezi wa haki za kibinadamu Boniface Akumu amepiga kambi katika mzunguko wa Kondele kushinikiza kurejeshwa kwa wakili Miguna Miguna nchini.

Akumu alieleza kuwa alikula mara ya mwisho Alhamisi, Machi 29, kabla kuanza kifungo cha kumtaka Miguna arudishwe nchini humo.

''Sijali hata kama nitakufa kutokana na njaa. Nimeudhika sana na jinsi serikali ilivyovunja sheria.’’Alisema.

Wengi wa wapita njia walifika katika mzunguko huo kumuona Akumu aliyekuwa amelala kando ya barabara akiwa na bango kubwa lenye ujumbe kwa serikali.
Na Geofrey Okechi.


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika Mashariki punde zinapojiri.
MTU MMOJA AAPA KUJIUA KISA MIGUNA MIGUNA - KENYA MTU MMOJA AAPA KUJIUA KISA MIGUNA MIGUNA - KENYA Reviewed by By News Reporter on 4/03/2018 02:19:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.