Loading...
Mwanasoka nyota wa kimataifa wa zamani Nwankwo Kanu ametangaza kwamba atawania urais katika uchaguzi mkuu mwaka 2019.
Kanu, aliyewahi kuzichezea Ajax, Inter Milan na Arsenal katika ujana wake, amesema ana ndoto ya kufanya mageuzi katika taifa hili kubwa na lenye watu wengi barani Afrika.
Mshindi huyo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 1995 hajaficha shauku yake ya kujiingiza katika siasa tangu alipostaafu kucheza soka akiwa klabu ya Portsmouth mwaka 2012. Kanu anaweza kufuata nyayo za gwiji wa soka George Weah ambaye sasa ni rais wa Liberia.
Wakati akitangaza nia yake ya kugombea urais, Weah – mshindi wa Tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika mwaka 1996 na 1999 aliwaambia wafuasi wake kadhaa.
Shauku ya urais wa Kanu
“Kuwepo kwangu hapa leo kunahusu hali ya baadaye ya nchi yetu na faraja ya watu wetu,” alisema mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 41.
“Miaka 18 iliyopita ya uongozi imeshuhudiwa kuanguka kwa sekta zote kubwa katika maisha ya Nigeria, pamoja na usalama katika ardhi hii. Pia, nitafanya kila liwezekanalo kupambana na ufisadi ambao umeenea kila mahali. Dunia inaitazama Nigeria kama makazi ya ufisadi.
“Ikiwa nitapewa mamlaka na ninyi, naahidi kufanya mambo tofauti na kurejesha heshima na maadili katika huduma za taifa kwa kuwa na watumishi bora na kuvutia walio bora.
"Ushindi wa George Weah nchini Liberia ni kielelezo kwamba ndoto hii inawezekana kwa ninyi wote kuwa upande wangu."
Kanu atakuwa anatarajiwa kuwa rais wa taifa hili ikiwa atafanikiwa kumshinda rais wa sasa Muhammadu Buhari.
Na Fatma Pembe.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.

MWANASOKA MKONGWE 'NWANKWO KANU' ATANGAZA KUWANIA URAIS NIGERIA 2019
Reviewed by By News Reporter
on
4/02/2018 01:34:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: