Loading...

NYOTA WA BOLLYWOOD 'SALMAN KHAN' AHUKUMIWA MIAKA 5 JELA KWA UJANGILI

Loading...

Mchezaji filamu nyota wa India (Bollywood) Salman Khan amehukumiwa kwenda jela miaka mitano kwa kosa la uwindaji haramu (Ujangili) wa tangu mwaka 1998.

Hukumu hiyo imetolewa na Mahakama ya Jodhpur ambapo pia amepewa adhabu ya kulipa Rupii 10,000 sawa na dola za Kimarekani 154; kwa kosa hilo.  Mwigizaji huyo sasa atapelekwa jela kuanza kifungo chake hicho kwa mujibu wa sheria.

Khan kanadaiwa aliua bata maji weusi wawili, viumbe ambavyo ni adimu na vinavyolindwa sana nchini humo, huko katika Jimbo la Rajasthan Magharibi wakati akitengeneza filamu.

Waigizaji wengine wanne ambao walikuwa pamoja na nyota huyo wakati wa kutengeneza filamu hiyo ambao alishitakiwa nao wameachiwa huru.

Hata hivyo Khan,mwenye miaka  52, anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Na Neema Joshua.

NYOTA WA BOLLYWOOD 'SALMAN KHAN' AHUKUMIWA MIAKA 5 JELA KWA UJANGILI NYOTA WA BOLLYWOOD 'SALMAN KHAN' AHUKUMIWA MIAKA 5 JELA KWA UJANGILI Reviewed by By News Reporter on 4/06/2018 11:14:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.