Loading...
Serikali ya Kenya kupitia Wizara yake ya Mambo ya Ndani imesema mwanamuziki wa Kongo, Koffi Olomide bado haitajiki nchini humo kwa kipindi cha miaka miwili baada ya kufukuzwa.
Ijapokuwa awali ilitaarifiwa kuwa, mkongwe huyo alithibitisha kupokea mwaliko wa kupiga shoo nchini humo kupitia Gavana wa Kakamega, Wycliffe Oparanya.
Kwa mujibu wa mtandao wa Citizen Digital la nchini Kenya, Olamide ni lazima aombe radhi ya kuondolewa vikwazo vya kutumbuiza Kenya, na hii kufuatia kisa cha kumpiga mmoja wa wanenguaji wake katika bendi yake katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyata (JKIA), Julai, 2016.
Koffi Olomide anatarajiwa kuwaburudisha mashabiki wake mjini Kakamega, wakati wa Kongamano la kila Mwaka la Tano la Ugatuzi, litakalofanyika Kata ya Kakamega kuanzia Jumatatu, Aprili 23 hadi Ijumaa, Aprili 27.
Na Fatma Pembe.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.

SHOO YA MWANAMUZIKI 'KOFFI OLOMIDE' NCHINI KENYA UTATA MTUPU
Reviewed by By News Reporter
on
4/15/2018 10:44:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: