Loading...
Wabunge wanne kati ya sita waliokuwa wakipatiwa matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) wameruhusiwa kurejea nyumbani.
Ijumaa Machi 30,2018 wabunge hao walilazwa MOI baada ya kupata ajali walipokuwa wakitokea Dodoma kuelekea Dar es Salaam.
Ajali hiyo ilitokea eneo la Bwawani mkoani Morogoro, Alhamisi Machi 29,2018 saa mbili usiku na kabla ya kuhamishiwa MOI walipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Morogoro.
Meneja Ustawi wa Jamii na Uhusiano wa MOI, Almas Jumaa akizungumza na gazeti moja hapa nchini jana Aprili Mosi, 2018 amesema mbunge wa Makunduchi, Haji Ameir Haji anaendelea na matibabu akiwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
Amesema Juma Othman Hija wa Tumbatu yupo wodini akiendelea na matibabu.
Na Catherine Kisese.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.

WABUNGE WANNE WALIOPATA AJALI WATOKA HOSPITALI
Reviewed by By News Reporter
on
4/02/2018 01:11:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: