Loading...
Wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa kuwasili nchini Tanzania kuangazia fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na sekta za Kilimo,Teknolojia na usafirishaji
Hayo yamebainika wakati Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier akizungumzia ziara ya siku tatu ya ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa wanaokwenda nchini Tanzania kuangazia fursa za kibiashara baina ya nchi hizo mbili.
Balozi Clavier ameongeza kuwa ujumbe huo utaongozwa na Shirikisho la Kimataifa la wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa MEDEF lenye wanachama 750,000 wakilenga kuwekeza katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na katika sekta za kilimo, Teknolojia ya habari na Mawasiliano na Mafuta na Gesi.
“Ziara hii yenye wakurugenzi 30 wa kampuni mbalimbali wanataka kushirikiana na Tanzania katika sekta za Usafiri ukiwemo wa anga na ardhini,TEHAMA,Kilimo ni miongoni mwa mengine” alisema Clavier.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Uchumi na Biashara wa Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania Beatrice Alperte amesema ukuaji wa teknolojia unakwenda sambamba na ukuaji wa uchumi kwa kuzingatia tafiti ndio maana wameamua kushirikiana na Tanzania katika kukuza uwezo wa watendaji.
Biashara kati ya Tanzania na Ufaransa imekua kwa wastani wa Dola za kimarekani milioni 30 ambapo Wafanyabiashara hao wanatarajia kukutana na Rais wa Tanzania Dkk.John Pombe Magufuli,Mawaziri katika sekta mbalimbali pamoja na viongozi wa sekta binafsi TPSF nchini.
Na Geofrey Okechi.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kitaifa punde zinapojiri.

WAFANYABIASHARA WA UFARANSA KUWEKEZA KATIKA, USAFIRISHAJI NA TEKNOLOJIA NCHINI
Reviewed by By News Reporter
on
4/12/2018 09:08:00 AM
Rating:
Reviewed by By News Reporter
on
4/12/2018 09:08:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: