Loading...

WAFUNGWA SABA WAUAWA KATIKA MAPIGANO JELA MAREKANI

Loading...
Wafungwa saba wameuawa na wengine 17 wamejeruhiwa katika mfululizo wa makabiliano katika jela la South Carolina, nchini Marekani, mamlaka imesema Jumatatu wiki hii.

Hali ya utulivu imerejea baada ya saa saba ya makabiliano katika jela la Bishopville, zaidi ya kilomita 60 kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa jimbo hilo, Columbia.

Makabiliano kati ya wafungwa yalienea kwa vyumba vitatu vya jela, ambapo watu karibu 1,600 wamefungwa.

Hii ni moja ya mapigano mabaya zaidi katika magereza ya Marekani kwa miaka mingi. Mnamo mwaka 1993, wafungwa watatu na afisa mmoja wa gereza waliuawa katika makabiliano katika jela la Lucasville, katika jimbo la Ohio.
Na Peter Godwin.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kimataifa punde zinapojiri.
WAFUNGWA SABA WAUAWA KATIKA MAPIGANO JELA MAREKANI WAFUNGWA SABA WAUAWA KATIKA MAPIGANO JELA MAREKANI Reviewed by By News Reporter on 4/17/2018 08:19:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.