Loading...
Serikali imewaonya watu wote au kikundi cha watu watakaothubutu kufanya uharibifu wa mabehewa ya treni ya abiria hususan wakati huu ambapo Serikali ipo katika mchakato wa kuliboresha Shirika la Reli nchini.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi ATASHASTA NDITIYE ametoa msimamo huo wa Serikali wakati alipotembelea Kituo cha Reli ya kati mkoani Tabora na kukagua mabehewa na karakana ya kurekebishia mabehewa ya treni ya abiria na mizigo.
NDITIYE ameonesha kukerwa kwake na tabia ya baadhi ya watu wanaofanya hujuma katika treni ya abiria ikiwemo kurusha mawe na kusababisha uharibifu mkubwa wa mabehewa ya abiria.
WAHARIBIFU WA MIUNDO MBINU YA TRENI WAONYWA
Reviewed by By News Reporter
on
4/28/2018 01:15:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: