Loading...

WANAWAKE WAADHIBIWA KUCHIMBA KABURI

Loading...
Ni kawaida na ni utamaduni wa sehemu nyingi duniani wanaume kuchimba kaburi na kuwaachia wanawake shughuli nyingine za jikoni wakati wa msiba.

Lakini sivyo ilivyokuwa kwa wanawake wa Mtaa wa Bwihegule wilayani Geita. Wanawake hao wa Kata ya Mtakuja walilazimika kuchimba kaburi, ikiwa ni adhabu iliyotokana na tuhuma kuwa wanahusika na vifo vya ghafla vya wanaume mtaani hapo.

Tukio hilo lililoibua hisia na maoni mchanganyiko kutoka kwa walioshuhudia lilitokea Aprili 24 baada ya mkazi wa mtaa huo, Nkangiko Vigume (57), kufariki dunia ghafla Aprili 23.

Habari kutoka mtaani hapo zinasema amri ya kutaka wanawake kuchimba kaburi na kulala matanga ilitolewa na mtemi, ambaye ni kiongozi wa mila wa jamii ya Wasukuma mtaani hapo, Kahema Nsabilando.

Alitoa amri hiyo baada ya uamuzi kufikiwa kwenye kikao cha dharura kilichojadili matukio ya vifo vya ghafla vya wanaume mtaani hapo.

Wakazi waliitisha kikao hicho kujadili vifo vya ghafla vya wanaume baada ya Vigume kufariki Aprili 23 na kufanya idadi ya waliokufa kufikia saba.
Na Peter Godwin.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kitaifa punde zinapojiri.
WANAWAKE WAADHIBIWA KUCHIMBA KABURI WANAWAKE WAADHIBIWA KUCHIMBA KABURI Reviewed by By News Reporter on 4/26/2018 09:27:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.