Loading...

AFA MAJI NIGERIA AKIJIPIGA 'SELFIE'

Loading...
MTU mmoja nchini Nigeria amefariki dunia baada ya kutumbukia katika mto wakati akijaribu kujipiga picha almaarufu 'Selfie'.

Kwa mujibu wa mtoto mmoja huko Nigeria, umeeleza kuwa tukio hilo limetokea eneo la Mto Nembe katika mji wa Bayelsa, ambapo jamaa huyo wa umri wa makamo kwa jina Taofeel alikua anajaribu kupiga picha ya mwisho ya kumbukumbu katika Chuo cha Mafunzo ya Usalama (NYSC).

Mtandao huo uliendelea kuandika kwamba bwana huyo aliteleza kwa bahati mbaya wakati walipokuwa amesimama eneo la Ogbolomabiri Jetty katika mto huo na kutumbukia mtoni.

Ripoti zaidi zinasema kuwa, mwili wa marehemu ulipatikana dakika 30 baada ya kuzama na hakuna taarifa za kumtambulisha zilizotolewa mara moja. 

Mamlaka za mji huo zimechapisha picha za marehemu na kuzisambaza katika mitandao mbalimbali ya kijamii ili kusaidia katika kumtambua.

Tukio la aina hii lilitokea Kenya Desemba, 31 2017, wakati mwanafunzi wa Chuo Kikuu Kabarak alipoteleza na kutumbukia mto Molo, Kaunti ya Nakuru selfies.
Na Geofrey Okechi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
AFA MAJI NIGERIA AKIJIPIGA 'SELFIE' AFA MAJI NIGERIA AKIJIPIGA 'SELFIE' Reviewed by By News Reporter on 5/08/2018 01:36:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.