Loading...

B GWAY ADAI NAY WA MITEGO MCHAWI

Loading...
Msanii wa Muziki wa Bongo fleva B Gway alijipatia umaarufu baada ya kutoa wimbo wake unaoitwa UNAJICHUKIA aliomshirikisha Nay wa Mitego amemgeuka Msanii huyo na kudai ni mchawi.

B Gway alikuwa msanii chini ya label ya Nay Free Nation lakini baada ya kuzinguana na kuondoka Kwenye label hiyo B Gway amedai hivi sasa Msanii huyo ameanza harakati za kumpoteza Kwenye gemu.

Kama utakumbuka siku za nyuma Nay alifanya shoo iliyotwa Nguvu ya kitaa maalumu kabisa kwa ajili ya kuchangisha pesa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko Dar lakini unaambiwa siku ya shoo mvua kubwa ilinyesha na B Gway anadai Nay alitumia nguvu za Giza kufukuza

Kwenye mahojiano aliyofanya na E-news ya East Africa Tv, B Gway alifunguka haya:

"Ile Nguvu ya kitaa tu vitu vingi viliendelea maana kulikuwa kuna bonge la mvua lakini pale Tanganyika Packers kulikuwa kukavuu."

"Unajua mimi naamini sana katika uwezo wa Mwenyezi Mungu yaani naamini sana kwamba nitafika kwa iyo kama yeye ana Imani atatia ubani mambo yangu yaharibike basi amekosea sana".
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
B GWAY ADAI NAY WA MITEGO MCHAWI B GWAY ADAI NAY WA MITEGO MCHAWI Reviewed by By News Reporter on 5/30/2018 12:36:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.