Loading...

CHAMELEONE NA SHEEBAH KUFANYA MATAMASHA SIKU MOJA; JE MBABE ATAKUWA NANI?

Loading...
Jose Chameleone na Sheebah kuonyeshana ubabe mwezi Novemba 30, watakapofanya matamasha yao siku moja! 

Wakisemwa kama ndio wasanii wakubwa kwa sasa, maswali mengi yanaulizwa "je nani ni nani?" lakini swali kubwa mpaka siku hiyo ni nani atajaza mashabiki wengi kuliko mwingine.
Chameleone anatarajiwa kufanya onesho lake katika viwanja vya Lugogo Cricket Oval wakati Sheebah anatarajiwa kukinukisha katika Klabu ya Rugby. Wasanii hao wawili hadi sasa haikuwa wazi kwanini waliamua kupanga tarehe moja ya matamasha yao.

Lakini hii sio mara ya kwanza kwa mwanamuziki Chameleone kufanya tamasha siku moja na msanii mwingine ilishawahi kufanyika mwaka 2015 alipofanya tamasha la kimuziki siku moja na mwanamuziki King Saha.

Hata hivyo, Promota wa Sheebah, Musa Kavuma anaonekana kuwa na wasi wasi kuwa huwenda siku hiyo biashara kwake ikawa mbaya baada ya kumuita Jose kama wanaweza kujadili swala hilo lakini Jose aligomea wito.
Na Fatma Pembe.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za burudani punde zinapojiri.
CHAMELEONE NA SHEEBAH KUFANYA MATAMASHA SIKU MOJA; JE MBABE ATAKUWA NANI? CHAMELEONE NA SHEEBAH KUFANYA MATAMASHA SIKU MOJA; JE MBABE ATAKUWA NANI? Reviewed by By News Reporter on 5/04/2018 12:06:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.