Loading...
Chanjo dhidi ya maradhi ya Ebola itaanza kutolewa hapo kesho katika maeneo ya vijijini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambako mripuko wa virusi vya Ebola uliripotiwa mapema mwezi huu.
Hayo yametangazwa na wizara ya afya huku idadi ya visa vilivyothibitishwa vya Ebola katika vijiji hivyo, vikiongezeka hadi 35 ikiwemo vifo 10.Kampeini ya chanjo tayari ilianza kutolewa katika mji wa Mbandaka ulio na idadi ya watu milioni 1.2 ambako maambukizi ya watu wanne yameripotiwa.
Takriban wahudumu 100 wa afya mjini humo wamepokea chanjo hiyo dhidi ya ebola.
Msemaji wa wizara ya afya Jessica Illunga amesema kampeini ya chanjo itaanza kesho Jumatatu katika vijiji vya Bikoro na Iboko kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
Shirika la afya duniani WHO limesema wiki chache zijazo zitakuwa muhimu katika kutathmini iwapo mripuko huo wa Ebola Congo unaweza kudhibitiwa au la.
Na Fatma Pembe.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

CHANJO YA EBOLA KUANZA KUTOLEWA BIKORO NA IBOKO JUMATATU
Reviewed by By News Reporter
on
5/27/2018 12:34:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: