Loading...

EMINEM AFUNGUKA BAADA YA UVUMI KUWA ANATOKA KIMAPENZI NA NICKI MINAJ

Loading...
Inawezekana kuwa marapa hawa wakubwa ulimwenguni wanatoka kimapenzi?

Kwa takribani siku kadhaa nyuma, uvumi ulitawala kila kona kuwa marapa maarufu Eminem na Nicki Minaj wanatoka kimapenzi, iliripotiwa na mtandao wa TMZ.

Hayo yote yalianzia wakati mashabiki wa Nicki Minaj walipomuuliza rapa huyo kupitia ukurasa wake Instagram kwamba, je anatoka kimapenzi na rapa Eminem au la. Alijibu NDIO!

Wakati wa Tamasha la Eminem hivi karibuni huko mjini Boston, US, rapa huyo aliwauliza mashabiki zake swala ambalo lilizidi kuwashangaza mashabiki hao kuhusu uhusiano wake na Nicki.

"Boston, ni wangapi kati yenu wanataka mimi nitoke kimapenzi na Nicki Minaj?" aliuliza.

"Vizuri, hata mimi pia nataka," alisema baada ya halaiki kujibu NDIO. "Nicki, kama umepata ujumbe, nitumie meseji baadae, tutalizungumzia vizuri."

Baada ya malkia wa rap kuona video hiyo katika mitandao ya kijamii, alijibu kwa meseji ya ukarimu.

"Lmfao. Ukweli ni kwamba ni shujaa na mkarimu kama nilivyo mimi. Nampenda sana," Nicki alisema.

Kwa mwenendo huo, inaonyesha rapa hawa wawili wamezimiana na watatoka kimapenzi.
Na Catherine Kisese.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
EMINEM AFUNGUKA BAADA YA UVUMI KUWA ANATOKA KIMAPENZI NA NICKI MINAJ EMINEM AFUNGUKA BAADA YA UVUMI KUWA ANATOKA KIMAPENZI NA NICKI MINAJ Reviewed by By News Reporter on 5/31/2018 10:20:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.