Loading...
Iran imekataa madai ya Israel kuhusu kuwepo kwa nyaraka za siri kutoka Tehran zinazothibitisha kuwa bado wanaendelea na mpango wao wa Nyuklia.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anasema kuwa nyaraka hizo zinaonesha kuwa Iran imeendelea na mpango wake wa Nyuklia hata baada ya kusaini mkataba wa mwaka 2015 wa kuachana na mpango huo.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa iran Imeendelea na mpango wake wa nyuklia mbali na kuwa iliahidi kwa jumuiya ya mataifa kuachana na masuala ya Nyuklia.
''Hata kutoka kwa mfano huu, unaweza kupata majibu ya aina nne, kwanza Iran imefanya ulaghai kuhusu kuachana na silaha za nyuklia, nyaraka zaidi ya mia moja zinaonesha hivyo, pili hata baada ya makubaliano ya kuacha, Iran imeendelea kutunza na kukuza mpango wake wa nyuklia kwa matumizi ya baadaye, tatu Iran imedanyanya tena mwaka 2015 na mwisho makubaliano yote yamejaa uongo mtupu'' Alisema Netanyahu.
Akiazungumza na wafanyakazi mjini Tehran kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei alikanusha madai hayo na kusema kuwa nchi yake itajibu kama Marekani itafanya maamuzi yoyote ya kuwaumiza.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa Netanyahu ametoa taarifa muhimu na suala la Iran kuendela na mpango wa nyulia haukabaliki.
Marekani inatarijiwa kutoa majibu ndani ya wiki mbili ikiwa wataweka vizuizi vyoyote dhidi ya iran.
Na Fatma Pembe.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kimatifa punde zinapojiri.

IRAN YAPINGA TUHUMA ZA KUENDELEA NA URUTUBISHAJI WA NYUKLIA
Reviewed by By News Reporter
on
5/01/2018 12:13:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: