Loading...

KIGWANGALLA AMTEUA MLIMBWENDE KUWA BALOZI

Loading...
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amemteua mshindi wa taji la Miss Journalism Tanzania, 2018, Witness Teddy Kavumo (21) kuwa balozi wa utalii wa Pori la Akiba Selous.

Dk Kigwangala alizungumza na mlimbwende huyo mwishoni mwa wiki alipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kuomba ufadhili wa kuandaa mradi wa kijamii ambao ni sehemu ya shindano atakaloshiriki la taji la Dunia la Miss Journalism 2018 litakalofanyika Oktoba 27 Jijini Arusha.

Tayari Dk. Kigwangalla amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania, Devotha Mdachi kuandika barua ya uteuzi kwa balozi huyo mpya sambamba na kumkabidhi hati ya uteuzi aweze kunadi vivutio vya utalii vya pori hilo.

Mbali na barua ya uteuzi, Waziri huyo amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Dk. James Wakibara kuandaa safari maalum ya balozi huyo kutembelea Pori la Akiba Selous kwa ajili ya kuona na kujifunza mambo yanayohusu hifadhi hiyo kwa ajili ya utangazaji.

Katika taarifa iliyotolewa na ofisi yake, balozi huyo atatembelea mapori mengine ikiwemo BBK (Burigi, Biharamulo na Kimisi) mkoani Kagera na Mpanga Kipengele mkoani Njombe ambapo atatumia fursa hiyo kufanya mahojiano na wasichana wa vijiji jirani na hifadhi hizo kwa ajili ya mradi wa kijamii.

Awali Witness aliomba kupewa fursa ya kuwa balozi wa Tanzania kwenye moja ya sekta ikiwemo Misitu, Nyuki au Utalii ambako angetumia nafasi hiyo kwa ajili ya kuitangaza misitu.

Mbali na kushikilia taji hilo, Witness amewahi kushinda mataji mengine manne ya kimataifa ya ulimbwende nchini Afrika Kusini anakosomea urubani kwa sasa.

Mataji hayo ni Miss Garden Route 2017, Miss Bees Cape Town 2017, na mataji mawili ya kimkoa ambayo ni Miss Asla Capetown 2017 na Miss Carnival Mosselbay 2017.

Kwa hapa nchini amewahi kushinda Miss Arusha Higher Learning 2014 na Miss Northern Zone 2014.
KIGWANGALLA AMTEUA MLIMBWENDE KUWA BALOZI KIGWANGALLA AMTEUA MLIMBWENDE KUWA BALOZI Reviewed by By News Reporter on 5/14/2018 08:36:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.