Loading...

MELI YA KUZALISHA UMEME KUTOKA UTURUKI YAWASILI NCHINI SUDANI

Loading...
Meli kutoka Uturuki yenye uwezo wa kuzalisha megawat 180 za umeme yawasili Sudani baada ya kusainiwa mkataba wa ushirikiano katika sekta ya nishati baina ya Uturuki na Sudani.

Meli hiyo yenye uwezo wa kuzalisha  megewatts 180 za umeme inatarajiwa kutoa  huduma ya umeme baada ya kusainiwa mkataba  na shirika la kuzalisha nishati ya umeme Sudani STPG.

Meli hiyo imewasili  katika bandari ya kimataifa ya Sudani na  tayari kwa kuanza kutoka  huduma ya umeme.

Shirika la  "Karpowership" ambalo lina miliki  "Karadeniz Powership Rauf Bey" limefahamisha Jumanne kuwa  meli hiyo imeanza kutoa huduma ya umeme tangu kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Meli hiyo ni miongoni mwa meli 6 za Uturuki ambazo zinztoa huduma ya umeme barani Afrika. Shirika hilo la uzalishaji wa umeme kutoka nchini Uturuki lina meli zake  ambazo zinatoa huduma ya umeme nchini Ghana, Msumbiji, Zambia, Gambia na Sierra Leone.

Na Paskali Joseph.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MELI YA KUZALISHA UMEME KUTOKA UTURUKI YAWASILI NCHINI SUDANI MELI YA KUZALISHA UMEME KUTOKA UTURUKI YAWASILI NCHINI SUDANI Reviewed by By News Reporter on 5/24/2018 11:17:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.