Loading...

MIMBA YA LULU YAMTOA GEREZANI

Loading...
Kwa sasa amekuwa akitumikia kifungo cha nje kinachomfanya baadhi ya watu wamuone kipindi anaingia na kutoka katika eneno lake husika analifanyia adhabu, hata hivyo kwa waliomuona Lulu wanadai kuwa mwana dada huyo anaonekana katika hali isiyo ya kawaida kutokana na mwili wake ulivyo.

Kwa waliomzoea Lulu wanasema kuwa mwanadada huyo ni mjamzito kwa sababu tumbo limekuwa kubwa kidogo lakini pia hata mwili wake hasa vidole vimevimba na pia mara nyingi amekuwa akionwa na watu akitema sana mate kitu kinachowafanya watu wengi kuamini kuwa inawezekana mwanadada huyo ni mjamzito na ndicho kilichomplekea kutoka gerezani.

Jitihada za kumtafuta ziligonga mwamba hasa baada ya lulu kukataa kuongea na waandishi wa habari kwa sababu bado hajamaliza kifungo chake ;lakini pia hataki kuongea na waandishi wahabari kwa sababu anataka kuanzia sasa maisha yake yawe ya kwake bila kushirikisha mitandao.

Waandishi hawakuishia hapo wakaona bora kutafuta  wazazi na watu wa karibu wa Lulu kuuliza kuhusu taraifa hizo ndipo walipojibu kuwa lulu sio mjamzito lakini hiyo ni hali ambayo anaweza kuwa nayo mtu yoyote hasa mtu aliyezoea kufanya mazoezi kisha akaacha kwa muda kama walivyoambiwa na daktari.

kutokana na hali hiyo sasa , watu wengi wamekuwa wanajipa majibu kuwa inawezekana msamaha wa lulu   kutoka kwa rais pia uliangalia sana hali yake ya kiafya.
Na Neema Joshua.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MIMBA YA LULU YAMTOA GEREZANI MIMBA YA LULU YAMTOA GEREZANI Reviewed by By News Reporter on 5/25/2018 09:38:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.