Loading...

JESHI LA NIGERIA LASHTUMIWA KUWABAKA WANAWAKE NA WATOTO

Loading...
Shirika la kimataifa linalotetea Haki za Binadamu, Amnesty International, linalishtumu jeshi la Nigeria kuwa limekuwa likiwabaka wanawake na watoto katika harakati zake za kuwasaka wanamgambo wa kundi la Boko Haramu Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Katika ripoti yake mpya Amnesty International inasema kuwa jeshi la serikali katika jimbo la Borno limehusika na vitendo vya ubakaji na kulazimisha suala la mahusiano na wanawake waliokimbia machafuko katika kambi za wakimbizi.

Hata hivyo ripoti imeendelea kueleza kuwa wanawake wanadhaniwa walikuwa wake wa wapiganaji wa Boko Haram watano kati yao wamefariki,huku watoto 32 wakidaiwa kufa pia.

Amnesty wanawatuhumu baadhi ya wanajeshi kufanya ukatili wa kingono dhidi ya wanawake katika kambi za wakimbizi wa ndani kama malipo kwa msaada wanaotoa.

Amnesty International inasema imefanya uchungui na kuweza kuhoji watu 250 kati ya mwaka 2016 na 2018.

Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema kuwa baadhi ya wanajeshi nchini Nigeria wanajinufaisha kimapenzi kwa kutumia mazingira magumu ya chakula yanayowawakabili wakimbizi hao.

Msemaji wa jeshi la Nigeria amefutilia mbali ripoti hiyo na kusema kuwa madai hayo hayana msingi wowote na ni uzushi unaolenga kupata matope jeshi la Nigeria.
Na Mohamedi Makame.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
JESHI LA NIGERIA LASHTUMIWA KUWABAKA WANAWAKE NA WATOTO JESHI LA NIGERIA LASHTUMIWA KUWABAKA WANAWAKE NA WATOTO Reviewed by By News Reporter on 5/25/2018 09:51:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.