Loading...

MWANAMUZIKI COYO APEWA KICHAPO KIZITO NA MASHABIKI KATIKA SHOO TARIME

Loading...
Mwanamuziki chipukizi wa  bongo fleva anayefanya vizuri na kibao chake cha Nyakanyaka, Coyo amedaiwa kutembezewa kipigo kizito na mashabiki zake kwenye shoo aliyofanya Tarime.

Shilawadu wanaripoti kuwa mwishoni mwa wiki iliyopita Coyo alikuwa anafanya shoo mbili moja Ikiwa ni Kenya na nyingine upande wa Tanzania kwa kuwa pale ni mpakani.

Lakini inasemekana alivyomaliza shoo ya Kenya alikuwa ana mpango wa kuwahi Tarime na kwenda kumaliza shoo ya Tanzania lakini usiku mnene ulikuwa umeshaingia hivyo alichelewa kufika na kukuta mashabiki wamevimba.

Unaambiwa alivyofika mashabiki hawakutaka maneno walianza kumtukana matusi mazito na ile anatoka nje wakamdaka wakampa kipigo kitakatifu mpaka Promota alipoenda kumuokoa.

Kwenye mahojiano na Soudy Brown, Coyo alikataa taarifa hizo na kudai kuwa hakuenda Kenya kufanya shoo bali alienda kusalimia marafiki lakini aliporudi kufanya shoo alitaka kufanyiwa utapeli na promota wa shoo yake.
Na Neema Joshua.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
MWANAMUZIKI COYO APEWA KICHAPO KIZITO NA MASHABIKI KATIKA SHOO TARIME MWANAMUZIKI COYO APEWA KICHAPO KIZITO NA MASHABIKI KATIKA SHOO TARIME Reviewed by By News Reporter on 5/05/2018 07:34:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.