Loading...

MZEE YUSUF APANGA KULIAMSHA DUDE

Loading...
Aliekuwa nguli wa muziki wa taarabu nchini, Mzee Yusup amefunguka na kusema kuwa siku yoyote hivi karibuni atalipua bomu la watu wanaokaa na kumnafikia huku wakijifanya kuwa wanapenda sana dini. Mzee Yusuph anasema kuwa kuna mtu ambae amekuwa akijuana nae kwa muda na anajua kuwa huyo mtu amekuwa ni moja ya watu anaowaamini na kuwa ameshika dini lakini kitu ch ajabu ni pale mtu huyo alipokuja na kumbadilikia kabisa kuhusu jambo fulani.

"kinachoniuma ni pale muislamu mwenzako anapokujia kidini kisha anakuja kukugeuka na kukuuliza kitu ambacho mpaka kiasi kwamba unakaa unajiuliza  karidati kwani, kiuhalisia io kila mtu wa kumuamini sana mpaka uishi nae muda mrefu kidogo ili umjue na wengine washenzi  mpaka uamini kuwa ni yeye  lakini mapka ukae nae kweli , kweli usimdharau usiemjua au usimuamini usiemjua."

Baada ya maneno hayo mashabiki wake walianza kutoa maoni na wengine kumpa pole huku wengine wakitaka kujua ni kitu gani kimemsibu baba huyo mpaka kuamua kusema maneno hayo yote ndipo aliposema tena.

"Mtanielewa tu Inshallah , ngoja bomu lilipuke  lbda Allah aniokoe , lakini siku hizi tatu kutoka leo lazima niweke wazi."
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MZEE YUSUF APANGA KULIAMSHA DUDE MZEE YUSUF APANGA KULIAMSHA DUDE Reviewed by By News Reporter on 5/07/2018 10:02:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.