Loading...

RAIS KENYATTA ATIA SAINI SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAONI

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametia saini mswada wa Sheria ya Uhalifu wa Kompyuta na Mtandaoni ya mwaka 2018 kuwa Sheria, hatua hii itatoa adhabu kali kwa watakaopatikana na makosa ya mtandaoni.

Sheria hiyo inatoa adhabu ya faini ya Milioni 100 (dola 50,000 za Marekani) au kifungo cha miaka miwili jela, au adhabu zote mbili, kwa atakayepatikana na kosa la uenezaji wa habari za uzushi.

Mtu atakayepatikana na kosa la kueneza taarifa ambazo zinaweza kuzua taharuki au kuzua vurugu atafun
Loading...
wa jela zaidi ya miaka kumi.

Hatua hiyo imepokelewa kwa hisia na maoni tofauti kwa watu mbalimbali ambapo kiongozi wa zamani wa chama cha wanasheria Kenya Apollo Mboya amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kifungu hicho kinaweza kuwapa watawala ‘uhuru’ wa kukandamiza vyombo vya habari.

Kwa upande mwingine shirika la kimataifa la kutetea uhuru wa wanahabari Committee to Protect Journalists (CPJ) nalo limekuwa likipinga uidhinishaji wa mswada huo.
Na Geofrey Okechi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
RAIS KENYATTA ATIA SAINI SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAONI RAIS KENYATTA ATIA SAINI SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAONI Reviewed by By News Reporter on 5/17/2018 08:07:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.