Loading...

RIPOTI MPYA YA HALI YA KIAFYA YA MZEE MAJUTO INDIA

Loading...
Zikiwa zimepita siku 19 tangu mkongwe wa vichekesho Bongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ apelekwe nchini India kwa matibabu, ripoti mpya ya afya yake imetoka.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari hapa nchini, Ashraf ambaye alijitambulisha kuwa ni mtoto wa Mzee Majuto alieleza kwamba, kwa sasa afya ya Mzee Majuto inaendelea vizuri, tofauti na alivyokuwa hapa nchini licha ya kwamba bado anaendelea na matibabu.

"Kwa sasa baba anaendelea vizuri kwa kweli, tumewasiliana na waliopo naye kule hospitalini India, wanasema hali yake imeanza kutengemaa tofauti na alivyokuwa hapa Bongo. Kwa sasa ni hayo tu, mengine familia itazungumza zaidi baadaye,” alisema Ashraf," alizema mtoto wa mzee majuto.
Na Neema Joshua.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
RIPOTI MPYA YA HALI YA KIAFYA YA MZEE MAJUTO INDIA RIPOTI MPYA YA HALI YA KIAFYA YA MZEE MAJUTO INDIA Reviewed by By News Reporter on 5/23/2018 09:45:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.