Loading...

VYONNE CHAKACHAKA: ALI KIBA NAMUONA KAMA MWANANGU

Mwanamuziki mkongwe kutoka Afrika ya Kusini Vyonne Chakachaka amefunguka na kuelezea ukaribu wake na msanii wa bongo Alikiba ambae kipindi cha nyuma kidogo walishawahi kuonekana kuwa pamoja wakiwa studio na kusemekana kuwa walikuwa wakitengeneza nyimbo mpya ya pamoja.

Vyonne ambae hivi sasa yupo nchini aliwahi kufanya mahojiano leo katika kipindi cha Clouds 360 katika clouds media na kuongea mengi lakini  hakusita kusema kuwa alikiba ni kama mwanae wa
Loading...
iume na meneja wa alikiba ambae ni Seven Mosha ni kama mtoto wake wa kike.

"Namuona alikiba kama mwanangu wa kiume na meneja wake ni kama mtoto wake wa kike, ninawapenda sana watoto wangu. na katika album yangu mpya inayokuja kuna wimbo nimeimba na alikiba na tuta-perform hivi kesho kwa mara ya kwanza," alisema Vyonne.

Siku ya kesho mwanamama Vyonne ataperform katika mkutano wa Africa Connect ambapo kwa mara ya kwanza wataimba wimbo wa pamoja na Alikiba kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.
Na Paskali Joseph.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
VYONNE CHAKACHAKA: ALI KIBA NAMUONA KAMA MWANANGU VYONNE CHAKACHAKA: ALI KIBA NAMUONA KAMA MWANANGU Reviewed by By News Reporter on 5/16/2018 03:32:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.