Loading...

WATU 5 WASHAMBULIWA NA MNYAMA NYATI

Loading...
Watu watano, wakazi wa Kata ya Kirongo, wilayani Rombo, Kilimanjaro wamelazwa hospitali baada ya kujeruhiwa na mbogo anayesadikiwa kutoka nchi jirani ya Kenya.

Majeruhi hao wamelazwa katika Hospitali ya Karume iliyopo tarafa ya Usseri wilayani humo.

Akizungumza na gazeti moja, jana Mei 14, Diwani wa kata ya Kirongo, Samanga Kimario amesema kuwa watu hao walikumbwa na mkasa huo wakati wakitoka kanisani jana Jumapili.

“Inasemekana walikuwa wanatoka kanisani na wakavamiwa na mnyama huyo na akawajeruhi sehemu mbalimbali za miili yao,” amesema
Kimario amesema kuwa mnyama huyo amezua taharuki kubwa na ya kihistoria kwani  haijawahi kutokea mbogo akaingia eneo hilo.

Pia amesema baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi aliwasiliana na maofisa wanyamapori ili kupata msaada zaidi wa kunusuru maisha ya wananchi.

"Baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi kuhusiana na mnyama huyo niliwasiliana na maofisa wanyamapori ili watusaidie na baadaye walifanikiwa kumuua mnyama huyo, " amesema Diwani Kimario.

Na Paskali Joseph.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
WATU 5 WASHAMBULIWA NA MNYAMA NYATI WATU 5 WASHAMBULIWA NA MNYAMA NYATI Reviewed by By News Reporter on 5/15/2018 01:34:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.