Loading...

ZAIDI YA ASILIMIA 85 AFRIKA AJIRA ZAO SIO RASMI RIPOTI YA ILO

Loading...
Shirika la Kazi duniani ILO linasema katika ripoti yake kuwa, watu Bilioni 2, sawa na asilimia 61 ya watu walioajiriwa, wapo katika ajira zisizo rasmi.

Ripoti ya ILO inaeleza pia kuwa, watu hao wanatoka katika mataifa yanayoendelea kiuchumi, huku wanawake wakiwa ni Milioni 740.

Barani Afrika, asilimia 85.8 ya ajira sio rasmi huku Asia ikiwa katika nafasi ya pili kwa silimi 68.2.

Aidha, ripoti hii iliyotolewa wakati dunia inaadhimisha sikukuu ya wafayakazi, inaeleza pia kuwa idadi kubwa ya watu wanaojihusisha katika ajira hizo zisizo rasmi ni wanaume, huku wanawake wakiwa ni asilimia 58.1.

Inaelezwa kuwa, kazi nyingi zilizo rasmi zinafanywa na watu wanaoishi katika maeneo ya vijijini.

Pamoja na hilo ukosefu wa elimu kwa watu wengi pia inachangiwa pakubwa kutokana na hali hii.
Na Paskali Joseph.




Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika punde zinapojiri.
ZAIDI YA ASILIMIA 85 AFRIKA AJIRA ZAO SIO RASMI RIPOTI YA ILO ZAIDI YA ASILIMIA 85 AFRIKA AJIRA ZAO SIO RASMI RIPOTI YA ILO Reviewed by By News Reporter on 5/01/2018 03:03:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.