Loading...

ASHANGAZA WATU KWA KUMZIKA BABA YAKE KWA GARI LA KIFAHARI, BMW

Loading...
Kuna njia nyingi za kufanya mazishi kwa mpendwa wako ila kwa huyu jamaa kutoka Nigeria, upande aliwashangaza na kuwaacha wengi midomo wazi.

Kufuatia picha na taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii, jamaa huyo alichukua gari mpya ya BMW na kumweka baba yake marehemu ndani, iwe kama jeneza kabla ya kulizika kwenye kaburi lenye urefu wa futi sita.

Jamaa huyo aliyetambulika kwa jina la Azubuike aliwashangaza wenyeji baada ya kuamua kufanya jambo kubwa kama ishara ya heshima kwa baba yake.

Ni kwenye hafla iliyohudhuriwa na wengi si tu kuomboleza naye bali kushuhudia tukio la ajabu pia.

Ilisemekana kuwa gari hilo lilinunuliwa kwa ajili ya kumzika babake na wala halikuwa limetumika.

Baadhi ya watu walimshutumu kwa kitendo hicho cha 'kijinga' wakisema kuwa ni jambo la kumkufuru mungu aliyemjalia utajiri huo.
Na Neema Joshua.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
ASHANGAZA WATU KWA KUMZIKA BABA YAKE KWA GARI LA KIFAHARI, BMW ASHANGAZA WATU KWA KUMZIKA BABA YAKE KWA GARI LA KIFAHARI, BMW Reviewed by By News Reporter on 6/11/2018 04:04:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.