Loading...

BABY MADAHA: SITAKI KUGAWA PENZI LANGU KWA WANAUME WAKIBONGO

Loading...
Msanii wa Bongo fleva Baby Madaha amewapa makavu ya Uso wanaume wa Dar na kudai ni Matapeli wa mapenzi. 

Baby Madaha amefunguka na kuwatolea uvivu wanaume wa Kibongo huku akiweka wazi kuwa kutoka na wanaume hawa ni kujitia tu nuksi kwani huishia kukupotezea muda na kukutosa. 

Kwenye mahojiano na mtandao mmoja wa hapa nchini ,Baby  Madaha alisema kuwa watu wengi hawamuelewi kwa nini hawajawahi kumuona na mwanaume au kumnadi mpenzi wake mitandaoni kwa sababu hapendi kabisa kutoka kimapenzi na Mbongo. 

Watakuja kunisikia tu nimeolewa huko nje ndio watajua ninachomaanisha, sipendi kabisa kumpa penzi Mmbongo kwa sababu wengi wababaishaji na wanajua kutiana nuksi sana kwakweli“. 

Wanaume wa Kibongo nao wamekuwa wakisema hayo hayo mambo kuhusu wanawake hadi wengine hasa mastaa wa kiume wameonekana wakienda kuoa nje ya nchi kwa kuwakimbia watoto wa kike wa kibongo.
Na Neema Joshua.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
BABY MADAHA: SITAKI KUGAWA PENZI LANGU KWA WANAUME WAKIBONGO BABY MADAHA: SITAKI KUGAWA PENZI LANGU KWA WANAUME WAKIBONGO Reviewed by By News Reporter on 6/03/2018 02:31:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.