Loading...

FAMILIA YA MSANII 'NASIB ABDUL' YAMWANGUKIA ZARI

Loading...
Habari iliyobamba katika mitandao jana na leo ni kuhusu video ya wimbo mpya wa Diamond Platnumz, Iyena, ambayo imeachiwa saa 22 zilizopita.

Kutoka kwa wimbo huo kumesababisha familia ya staa huyo kutumia fursa ya kumuangukia aliyekuwa mpenzi wake, Zari Hassan na kuzua mjadala katika mitandao.

Katika mtandao wa Instagram, mama mzazi wa mwanamuziki huyo, Sanura amekuwa akiweka picha akiambatanisha na maneno ya kumsifu mwanamke huyo anayeishi nchini Afrika Kusini.

Mwingine kutoka familia ya Diamond aliyeshiriki katika mjadala huo ni dada yake, Esma ambaye amemsifu wifi yake huyo wa zamani kwa usafi.

Esma alizua mjadala zaidi baada ya kumtaja wifi yake mwingine wa zamani Wema Sepetu, akisema ni bingwa wa kupika misosi mitamu.

Wapo ambo wanaojiita timu Hamisa waliomtetea mwanamitindo huyo wakimtaka Diamond arekodi upya video hiyo kwa kuwa hiyo imefanyika Septemba mwaka jana kabla ya Zari kutoa tamko la kuachana na mzazi mwenzake huyo.
Na Neema Joshua.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
FAMILIA YA MSANII 'NASIB ABDUL' YAMWANGUKIA ZARI FAMILIA YA MSANII 'NASIB ABDUL' YAMWANGUKIA ZARI Reviewed by By News Reporter on 6/02/2018 09:47:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.