Loading...

KILICHOSABABISHA NDOA YA MCHEKESHAJI 'KANSIIME' KUVUNJIKA

Loading...
Mchekeshaji maarufu kutoka Uganda, Ann Kansiime amedai kuwa huenda mumewe alimuacha kwa sababu alikuwa akitengeneza pesa nyingi kumzidi.

Kansiime aliwashangaza wafuasi wake Novemba 1, 2017 alipotangaza kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba yeye na mumewe Gerald Ojok walikuwa wametengana.

Kulikuwa na tuhuma kwamba Ojok alimuacha Kansiime kwakuwa alikuwa hana uwezo wa kuzaa watoto ila Kansiime mwenyewe alikuwa na kauli tofauti.

Kwa mujibu wa Kansiime ambaye alikuwa Kenya mwisho wa juma lililopita, Ojok alimuacha kwa sababu kadhaa na ambazo zingine asingependa kuzizungumzia.

Kansiime alifichua kwamba uhusiano wake wa kimapenzi na Ojok uliisha miezi sita kabla ya yeye kuamua kuvunja ukimya wake kwenye ukurasa wa Facebook Novemba 1, mwaka jana.

Aidha mchekeshaji huyo alidai kuwa amekuwa mpweke kwa muda mrefu na sasa anatafuta mume ambaye atampenda jinsi alivyo na wafunge pingu za maisha.
Na Fatma Pembe.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
KILICHOSABABISHA NDOA YA MCHEKESHAJI 'KANSIIME' KUVUNJIKA KILICHOSABABISHA NDOA YA MCHEKESHAJI 'KANSIIME' KUVUNJIKA Reviewed by By News Reporter on 6/12/2018 08:18:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.