Loading...

LAZIMA NICHUKUE BALLON D'OR HAPA JUVE

Loading...
MCHEZAJI bora wa dunia Cristiano Ronaldo, amesema ni jambo zuri yeye kusaini kuichezea Juventus badala ya kwenda China au Qatar.

Ronaldo alitambulishwa kwenye timu yake mpya juzi baada ya kukaa Real Madrid kuanzia mwaka 2009, alipojiunga na timu hiyo akitokea Manchester United.

Akiwa Madrid, Ronaldo alifanikiwa kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mara nne.

“Kuja kwenye timu hii kwa kipindi hiki ni jambo la kufurahisha sana,” alisema Ronaldo wakati anatambulishwa mjini Turin.

Ronaldo alisema kuwa yeye ni mchezaji mwenye bahati sana kupata nafasi ya kujiunga na Juventus kwa kuwa ni timu kubwa Ulaya kwa sasa. Ronaldo alifanikiwa kufunga mabao 450 akiwa na Real Madrid pamoja na kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mara nne, pia alitwaa La Liga mara mbili na makombe mengine makubwa.

“Nataka kushinda, nataka kuwa bora, nani anafahamu? Labda naweza kutwaa tena tuzo ya mchezaji bora wa dunia ‘Ballon d’Or’ nikiwa kwenye timu hii,” alisema.
Na Haika Gabriel.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
LAZIMA NICHUKUE BALLON D'OR HAPA JUVE LAZIMA NICHUKUE BALLON D'OR HAPA JUVE Reviewed by By News Reporter on 7/18/2018 11:37:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.