Loading...
Mama mzazi wa aliyekuwa staa wa Bongo movie Steven Kanumba, Flora Mtegoa maarufu kama Mama Kanumba amemtaja msanii ambaye anaamini ameziba pengo la Kanumba Kwenye tasnia ya Bongo movie.
Mama Kanumba ambaye naye aliingia Kwenye Bongo Movie mara baada ya mwanaye kufa amemtaja Gabo Zigamba kama Msanii ambaye ameziba pengo la Kanumba.
Kwenye mahojiano na Wasafi TV, Mama Kanumba amemtaja Muigizaji wa Kiume Gabo Zigamba kama ndiye msanii pekee mwenye uwezo sawa na Kanumba kwa sasa.
"Gabo anajitahidi kwa kweli, nilichogundua kwanza anajua kuuvaa uhusika kwenye filamu zake, akiwa kama mlinzi anakuwa mlinzi kweli, akiwa kichaa anakuwa kichaa kweli. Namwambia asikate tamaa kuna watu watamkatisha tamaa kila atapokaribia kuyafikia mafanikio zaidi."
Lakini pia Mama Kanumba amelinganisha uwezo wa Kanumba na Gabo:
"Ni kweli Gabo ‘anashika kijiti cha Kanumba’ anajitahidi, anauthubutu, anajaribu, anajituma na anaweza".
Na Neema Bushubo.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

MAMA KANUMBA ADAI GABO AMEFANIKIWA KUZIBA PENGO LA MWANAE KANUMBA
Reviewed by By News Reporter
on
7/23/2018 10:40:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: