Loading...

MAMBO 11 YANAYOATHIRI UBONGO NA KUKUNYIMA UWEZO WA KUKUMBUKA NA KUFIKIRIA VIZURI

Loading...
Tunatumia ubongo kufikiria na kuendesha shughuli nyingi kama binadamu ikiwemo masomo, hivyo ubongo unahitaji lishe bora na kuepushwa na kemikali hatari.

Kitu chochote kinachotatiza ubongo na kuuharibu kinaweza kuwa hatari kwa maisha ya binadamu.

DundiikaNews imekuandalia tabia 11 ambazo zinaweza kuuharibu ubongo wako na kukuathiri pakubwa:

1. Kukosa kupata kiamsha kinywa 

Chakula cha asubuhi ni muhimu zaidi kwa mwili sana kwa kuwa kinausaidia ubongo kurejelea kazi yake ya kuudhibiti mwili na kuendeleza udhabiti wa kihisia. 

Kukosa kiamsha kinywa kunaweza kusababisha ukosefu wa nguvu kwa ubongo, kukosa kuwa makini na kutokumbuka, utendakazi duni na udhaifu wa mwili. 

Kunywa kati ya vikombe vitatu au vine vya kahawa kila siku ili kuimarisha hali yako ya kukumbuka na kukuepusha na magonjwa ya Alzheimer na Parkinson.

2. Kuvuta sigara 

Uvutaji wa sigara mara kwa mara hupunguza kiwnago cha seli za ubongo na hewa ya oksijeni inayotumika kwenye ubongo. 

Imedhibitishwa kuwa uvutani wa sigara huathiri ubongo kwa magonjwa kama Alzheimer. Kemikali kwa jina ‘heterocyclic amines’ ambazo hutokea kwenye sigara husababisha kuchipuka kwa seli za saratani mwili zinazoathiri ubongo.

3. Kutumia sukari na vyakula vyenye sukari kwa wingi 

Kutumia sukari zilizosindikwa, unga mweupe, vyakula vilivyokaangwa na vile vilivyopakiwa bila ya kuchanganya na mboga na matunda huingiza kemikali hatari mwilini. 

Kemikali hizo husababisha kukua kwa choa au kivimbe mwili kinachotatiza hali ya kawaida ya mwili, inasababisha afya duni na kuhitilafiana kwa mfumo wa fahamu mwilini na ukuaji wa viungo muhimu. 

4. Kuwepo kwenye mazingira yaliyochafuliwa mara kwa mara 

Ubongo unahitaji oksijeni mara kwa mara, hivyo hewa iliyo na chembechembe za kemikali hatari husafirishwa hadi kwenye ubongo na kuathiri utendakazi wake inavyostahili. 

5. Kukosa kulala vya kutosha 

Binadamu anahitaji saa nane za kulala ili kuiwezesha ubongo kupumzika, kuupa mwili muda wa kuendeleza usagaji wa chakula na kuimarisha seli. Kukosa usingizi kunachangia kufa kwa seli za ubongo na kumfanya mtu kuwa mchovu siku nzima na kukosa kuwa mchangamfu.

6. Kula kupita kiasi 

Kula chakula kupita kiasi kunasababisha vyakula vya ziada kuhifadhiwa kama mafuta mwilini, hivyo kuathiri mishipa tofauti na mwishowe kuathiri utendakazi wa ubongo na sehemu za mwili.

7. Kunywa pombe 

Pombe huathiri viungo vyote, mfumo wa neva, figo na moyo. Hali hiyo husababisha mchanganyiko wa kemikali kadhaa kwenye ubongo na kuuathiri. 

Pombe pia huziangamiza seli za neva zinazosafirisha mawasiliano ya mipigo mwilini na kupunguza kasi ya mipigo hiyo.

8. Hisia za hasira, kutatizika kiakili na kimawazo 

Kutatizika kiakili na kimawazo, haswa msongo wa mawazo husababisha ubongo kupunguza kasi yake ya kufanya kazi, hali ambayo humweka mtu kwenye hatari ya kupata mshuko wa moyo au kiharusi. 

9. Kufunika uso unapolala 

Kuufunika uso wako unapolala kunaongeza kiwango cha hewa ya dioksidi kabonia, yaani ‘carbon dioxide’ na kupunguza oksijeni, hali ambayo inaweza kuathiri ubongo wako.

10. Kujilazimisha kufanya kazi unapokuwa mgonjwa 

Kufanya kazi wakati mtu ni mgonjwa kunaharibu ubongo, kwani nguvu za mwili zinazostahili kuelekezwa kwa kumponya zinaelekezwa kwenye ubongo. 

Kufanya kazi ukiwa mgonjwa kunapunguza kinga ya mwili, husababisha magonjwa mengine na kupunguza ubora wa jinsi ubongo wako unavyofanya kazi. 

11. Kukosa kufanya mazoezi ya kimwili na kiakili 

Kuwa na mawazo, kuwa na mazungumzo yanayokuhitaji kutumia akili, kusoma kitabu, kutafuta neno huuchochea ubongo wako, huongeza uwezo wako kujifunza vitu vipya na kuvihifadhi akilini pamoja na kuimarisha kasi nzuri ya hisia zako kwa hali au matukio fulani.

NA Marry Mkeu.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MAMBO 11 YANAYOATHIRI UBONGO NA KUKUNYIMA UWEZO WA KUKUMBUKA NA KUFIKIRIA VIZURI MAMBO 11 YANAYOATHIRI UBONGO NA KUKUNYIMA UWEZO WA KUKUMBUKA NA KUFIKIRIA VIZURI Reviewed by By News Reporter on 8/01/2018 10:22:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.