Loading...
Mtandao maarufu wa kuuza miziki wa nchini Marekani, Spotify umemjibu Nicki Minaj kufuatia shutuma alizotoa staa huyo kwamba hawajatangaza albamu yake mpya ya 'Queen' kwa sababu alitambulisha albamu hiyo kwa mshindani wao.
"Spotify bado tunamuunga mkono Nicki Minaj katika mizunguko minne ya billboard, kumtangaza na kucheza muziki wake katika playlist kubwa, kipindi cha Miziki mipya ya Ijumaa, na chati ya miziki mipya," mwakilishi wa kampuni hiyo alisema katika tamko hilo.
"Wimbo wake mpya 'Bed' kiuhalisia inapanda juu kulingana na matangazo tunayofanya achilia mbali kampeni tuzifanyazo." Kampuni itaendelea kuwa mashabiki wakubwa wa Nicki.
Kufuatia mfululizo wa malumbano wa jumbe za twitter jana, Nicki aliishutumu Spotify kwa kutotangaza albamu yake, ijapokuwa walimuhaidi hilo, kwa sababu alitangulia kuitangaza nyimbo hiyo kupitia radio ya 'QueenRadio' ambayo inapatikana Apple Beats dakika kumi kabla ya kuipereka Spotify.
Albamu ya Minaj Queen inashikilia namba 2 katika chati 200 za Billboard nyuma ya Travis Scott anayetamba na albamu ya Astroworld.
Na Neema Joshua.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

MTANDAO WA SPOTIFY WAKANUSHA SHUTUMA ZA NICKY MINAJ KUHUSIANA NA KUTOTANGAZA ALBAMU YAKE MPYA
Reviewed by By News Reporter
on
8/22/2018 10:37:00 AM
Rating:
![MTANDAO WA SPOTIFY WAKANUSHA SHUTUMA ZA NICKY MINAJ KUHUSIANA NA KUTOTANGAZA ALBAMU YAKE MPYA](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgmgheP6D9Ayd7RbHzxmhyphenhypheniBH-TOCjArSfxEqyPwiRo1pElyxmK-DeTw0yIGdvhzIx2WFwO3yYlH_2xekR2fqgIqRD8YnaobzhhIr_e72l_VtzfQwjf8U0UbGiTBknbzh0l3Xr655td32A/s72-c/nicki+minaj.jpg)
Hakuna maoni: