Loading...
Mwanariadha maarufu aliyestaafu na mwanambio wa mita 100, mita 200 na relay mita 4 × 100 amejiunga na klabu ya kandanda ya Australia Central Coast Mariners kupata mazoezi kwa muda usiojulikana.
Tangu mwanariadha huyo aliye na umri wa miaka 31 alipostaafu, ametangaza wazi kwamba alilenga kujiunga na kandanda. Amefanya mazoezi na vilabu kadhaa ikiwemo ni pamoja na Borussia Dortmund na Mamelodi Sundowns FC.
Klabu ya Ligi A, Central Coast Mariners kilithibitisha hayo katika mtandao wa kijamii.
"Klabu ya Central Coast Mariners leo kinathibitisha kuwa Usain Bolt amejitolea kufanya mazoezi kwa muda usiojulikana kwa lengo la kuwa mwanakandanda.
"Makubaliano kati ya Central Coast Mariners na Usain Bolt hata hivyo hayatoi uhakika ikiwa atapata kandarasi ya kucheza kitaalam, lakini inatoa nafasi kwake kutimiza azimio lake la kucheza kandanda ya kitaalam,” ilisema klabu hiyo.
Bolt alipata umaarufu wake baada ya kushinda mara mbili na kuvunja rekodi ya dunia wakati wa mashindano ya Olimpiki ya Beijing 2008.
Alikuwa mtu wa kwanza kuvunja rekodi mara mbili wakati mmoja baada ya kushinda mita 100 na mita 200 mwaka huo wa 2008.
Alishinda mbio hizo tena 2012 na 2016.
Na Hamisi Fakhi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

MWANARIADHA USAIN BOLT AIBUKIA KATIKA SOKA RASMI
Reviewed by By News Reporter
on
8/08/2018 09:15:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: