Loading...

MZEE WA MIAKA 78 AUKATAA UBACHELA, AMUOA MWANAMKE WA MIAKA 60

Loading...
Kweli ng'ombe azeeki maini, ilikuwa vifijo na nderemo katika Kanisa la St Marks ACK, Kaunti ya Murang'a - Kenya, wakati mzee wa miaka 78 alipofanya harusi na mwanamke wa miaka 60, Jumapili Agosti 19.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na marafiki, jamaa na wapita njia waliofika kushuhudia kioja Ayub Mugo na Teresiah Njoki wakifunga pingu za maisha.

Kulingana na Daily Nation ya nchini humo, Mugo Jumapili Agosti 20 alionekana kuchoka kukaa peke yake kwa takriban miaka 10 alimuoa mama huyo.

Alisema kuwa uhusiano huo ungempa furaha maishani, “Mwaka wa 2017 nilipokuwa katika biashara yake binafsi huko Thika, niliona mwanamke ambaye alionekana kuwa maalum sana kwangu, nilihisi upendo mwingi na nikaamua kumfuata,” alieleza ‘guka’ huyo.

Alieleza kuwa alihisi sauti ikimshauri kumfuata mwanamke huyo kwa sababu huenda angekuwa mtu spesheli katika maisha yake.

“Nilisimama na nikamwalika kwa kikombe cha chai, alikubali. Tukiwa hotelini, nilipeana nambari za simu na baadaye tukajuana zaidi, baada ya siku kadhaa,” alisema.

Baada ya siku ya kwanza kukutana, babu huyo alieleza kuwa hakuwa na shaka kwamba angeaga kwaheri ‘ukapera’ karibuni.

“Nilijua kuwa angenipenda kwa sababu nilizidi kumwombea,” alisema Mugo na kuongeza kuwa aliwaita watoto wake watano na kuwaeleza kuhusiana na suala hilo ambapo walikubali. 

Ingawa bibi harusi mara za mwanzo alijaribu kukataa, alikubali hatimaye baada ya kuomba.
Na Catherine Kisese.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MZEE WA MIAKA 78 AUKATAA UBACHELA, AMUOA MWANAMKE WA MIAKA 60 MZEE WA MIAKA 78 AUKATAA UBACHELA, AMUOA MWANAMKE WA MIAKA 60 Reviewed by By News Reporter on 8/21/2018 08:13:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.