Loading...

VISA NA MIKASA: KISA NYETI MWANAMKE MMOJA AHUKUMIWA MIAKA 8 JELA

Loading...
Mahakama moja ya Eldoret, Kenya imempa mwanamke wa umri wa makamo kifungo cha miaka nane jela baada ya kupatikana na kosa la kumkata uume mumewe alipokuwa amelala.

Mahakama ilisikia kuwa Erica Iminza alimkata uume John Kisanya Mei 22, 2018 kwa kutumia kisu chenye makali.

Kwa kutoa hukumu hiyo, Hakimu Mkuu wa Eldoret Charles Obulutsa alisema waendeshaji mashtaka walikuwa wamewasilisha ushahidi wa kutosha dhidi ya mshukiwa.

Kulingana na eDaily, Kisanya alisema alifurahishwa sana na uamuzi huo. Mwanamume huyo ambaye alitafuta msaada wa matibabu katika Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Moi alieleza kuwa alijaribu sana kumaliza kesi hiyo nje ya mahakama, lakini juhudi zake zilitatizwa na familia ya mkewe. 

Mama huyo wa watoto wawili ana siku 14 kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
Na Hamisi Fakhi.





Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
VISA NA MIKASA: KISA NYETI MWANAMKE MMOJA AHUKUMIWA MIAKA 8 JELA VISA NA MIKASA: KISA NYETI MWANAMKE MMOJA AHUKUMIWA MIAKA 8 JELA Reviewed by By News Reporter on 8/21/2018 07:58:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.