Loading...

MMOJA AUAWA NA WENGINE WAJERUHIWA VIBAYA SAKATA LA BOBI WINE

Loading...
Mtu mmoja ameuawa na wengine watano kujeruhiwa katika mji wa Mityana baada ya polisi siku ya Jumapili kukabiliana na wafuasi wa mbunge wa upinzani Francis Zaake, baada ya ripoti kuwa hali yake ya afya ni mbaya.

Zaake ni mmoja wa wanasiasa wa upinzani waliokamatwa na kuzuiwa na wanajeshi katika mji wa Arua wiki iliyopita, baada ya kutoka kwa machafuko ya kisiasa na msafara wa rais Yoweri Museveni kurushiwa mawe.

Wanasiasa hao wanadaiwa kupigwa na kujeruhiwa vibaya na wanajeshi baada ya kukamatwa, akiwemo Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine ambaye amezuiwa kwenye kambi ya jeshi.

Kyagulanyi ni mwanasiasa mwenye umri wa miaka 36 ambaye umaarufu wake unaelezwa na wachambuzi wa siasa kuwa unampa tumbo joto rais Yoweri Kaguta Museveni na mwanasiasa mkongwe wa upinzani Kizza Besigye.
Na Geofrey Okechi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MMOJA AUAWA NA WENGINE WAJERUHIWA VIBAYA SAKATA LA BOBI WINE MMOJA AUAWA NA WENGINE WAJERUHIWA VIBAYA SAKATA LA BOBI WINE Reviewed by By News Reporter on 8/21/2018 07:43:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.