Loading...

RAIS KIIR WA SUDANI KUSINI ATOA MSAMAHA KWA MACHAR NA MAKUNDI YA WAASI

Loading...
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, ametangaza msamaha kwa makundi yote ya waasi akiwemo hasimu wake Riek Machar ambaye ni kiongozi wa waasi hao.

Kiir ametoa tangazo hili kupitia redio ya taifa, siku chache baada ya kutia saini mkataba wa amani wa namna ya kugawana madaraka na Machar jijini Khartoum nchini Sudan.

Msamaha huu unaanza tayari umeanza kutekelezwa.

“Rais Salva Kiir ametoa msamaha dhidi ya Dokta Riek Machar na makundi mengine ya waasi ambayo yamekuwa yakipambana na serikali tangu mwaka 2013. Msamaha huu unaanza kutekelezwa kuanzia tarehe 8 mwezi Agosti 2018,” Tangazo lililosomwa kupitia Redio ya Taifa.

Aidha, Kiir amewataka wanajeshi wanaomuunga mkono kutekeleza mkataba wa kusitisha makabiliano yoyote dhidi ya vikosi vya Machar.

Mkataba wa mwisho unatarajiwa kutiwa saini hivi karibuni,ili kuruhusu kuundwa kwa serikali ya mpito itakayoundwa baada ya miezi mitatu na kuongoza kwa miezi 36 kabla ya Uchaguzi Mkuu kufanyika.

Riek Machar, anatarajiwa kurejea katika wadhifa wa Makamu wa kwanza wa rais.
Na Geofrey Okechi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
RAIS KIIR WA SUDANI KUSINI ATOA MSAMAHA KWA MACHAR NA MAKUNDI YA WAASI RAIS KIIR WA SUDANI KUSINI ATOA MSAMAHA KWA MACHAR NA MAKUNDI YA WAASI Reviewed by By News Reporter on 8/10/2018 09:16:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.