Loading...

SENETA MAARUFU 'JOHN McCAIN' WA MAREKANI AFARIKI DUNIA

Loading...
McCain ambaye alikuwa anaugua saratani ya ubongo, alifariki katika chumba chake cha mapumziko mjini Sedona, Arizona, akiwa amezungukwa na familia yake.

Mwanasiasa huyo mkongwe aligunduliwa kuwa na ugonjwa huo hatari mnamo mwezi Julai mwaka 2017.

Famila ya McCain ilitangaza Ijumaa kwamba alikuwa amesitisha tiba "kwa sababu saratani imeenea sana."

Hadi kifo chake, McCain alikuwa anawakilisha jimbo la Arizona katika seneti ya Marekani.

Atakumbukwa kama mmoja wa mashujaa wa vita vya Vietnam na mmoja wa wanasiasa wachache walioshikilia misimamo yao kwa dhati bila kujali misingi ya vyama.

Alishikiliwa kwa miaka mitano kama mateka wa kivita nchini Vietnam kabla ya kurejea Marekani na kujitosa kwa siasa.

Alihudumu katika bunge la Marekani kwa miongo mitatu na aliwahi kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican mara mbili, na kuteuliwa kama mgomea rasmi mwaka wa 2008 ambapo alipambana na kushindwa na mgombea wa chama cha Demokratic, Barack Obama.

Punde tu baada ya habari za kifo chake kuchipuka, viongozi wa tabaka mbalimbali walianza kutuma jumbe za hususan kupitia mitandao ya kijamii, wengi wakimtaja kama shujaa.

"Tumempoteza shujaa shupavu," aliandika aliyekuwa mgombea mwenza wa urais, Sarah Palin kwenye Twitter.

"Nilikuwa na baba yangu wakati aliaga dunia," alisema mwanawe McCain, Meghan McCain.

Rais Trump aliandika kwenye Twitter: "Maombi yangu yaindee familia ya Seneta McCain."

Jumamosi jioni, bendera ya Marekani kwenye ikulu, White House, iliteremshwa nusu mlingoti kwa heshima ya mwanasiasa huyo.

McCain alizaliwa mwaka wa 1936 na aliwahi kuhudumu katika jeshi la wanamji kabla ya kuingia kwenye jeshi la wanahewa.

Amemwacha mjane, watoto saba, mama yake na wajukuu watano.
Na Catherine Joshua.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
SENETA MAARUFU 'JOHN McCAIN' WA MAREKANI AFARIKI DUNIA SENETA MAARUFU 'JOHN McCAIN' WA MAREKANI AFARIKI DUNIA Reviewed by By News Reporter on 8/26/2018 10:18:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.