Loading...

UCHAGUZI: GHASIA ZAZUKA NCHINI ZIMBABWE

Loading...
Ghasia zimezuka nchini Zimbabwe kati ya wafuasi wa upinzani na vikosi vya usalama katika mji mkuu wa Zimbabwe huku kukiwa na maandamano dhidi ya kucheleweshwa kwa matokeo ya uchaguzi

Magari yaliobeba maji ya kuwatawanya waandamanaji na vitoa machozi yalitumiwa katika barabara muhimu za mji wa Harare baada ya wafuasi wa chama cha upinzani cha MDC Alliance kuweka vizuizi katikati ya mji huo.

Mtu mmoja aliyekuwa miongoni mwa waandamanaji ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi. Muungano wa Ulaya umeonyesha wasiwasi wake kuhusu kucheleweshwa kwa matokeo.

Maandamano hayo ya wafuasi wa chama cha upizani cha MDC mjini Harare yalibadilika na kuwa mabaya nyakati za mchana.

Makundi ya waandamanaji yalikuwa katikati ya mji huo tangu alfajiri lakini habari zilipozuka kwamba Zanu Pf imeshinda viti vingi katika bunge na kwamba matokeo ya urais hayakuwa tayari , hali ilibadilika.

Walifanya maandamano katika barabara muhimu mjini Harare na kuelekea katika ofisi za zamani za chama cha Zanu Pf wakibeba mawe makubwa , fimbo na chochote kila ambacho wangeweza kubeba.

Kundi hilo lilisema 'tunamtaka Chamisa', wanaamini kwamba uchaguzi huo umekumbwa na udanganyifu na sasa wanataka mgombea wa MDC kutangazwa mshindi.

Matokeo yanaonyesha kwamba Zanu-PF inashinda viti vingi vya ubunge katika uchaguzi huo tangu kung'atuliwa madarakani kwa Robert Mugabe.
Na Paskali Joseph.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
UCHAGUZI: GHASIA ZAZUKA NCHINI ZIMBABWE UCHAGUZI: GHASIA ZAZUKA NCHINI ZIMBABWE Reviewed by By News Reporter on 8/02/2018 07:17:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.