Loading...
Tunaishi katika dunia ambayo kwa sasa ni rahisi sana mtu kuahidi jambo huku ndani akijua kabisa hana nia ya kutekeleza. Wakati ambao ni rahisi kwa mtu kutamka kwa maneno kuwa atafanya jambo fulani huku akijua bayana kabisa hatafanya jambo hilo.
Tumefika hatua ya kujiahidi wenyewe kuwa tutafanya jambo fulani katika maisha yetu huku kwa ndani kukiwa hakuna nia ya kuyafanya jambo hilo . Watu tumekuwa wepesi wa kuishi kwa maneno zaidi ya vitendo.
Mwenendo huu umekuwa tabia na jambo la kawaida katika baadhi yetu. Hili ni moja ya tatizo na kikwazo kikubwa katika kuboresha maisha yako kwa sababu umezoea kuweka ahadi kuwa utachukua hatua kisha hufanyi chochote.
Tabia hii pia inagharimu kupoteza kuaminika kwa watu wanaokuzunguka kutokana na kutoa ahadi usizotekeleza. Kumbuka, mafanikio yako yanategemea mchango wa watu wengine.
Maisha yako yatabadilika mara moja pale utakapoanza kutekeleza kila ahadi unayojiwekea mwenyewe na zile unazotoa kwa watu wengine. Jifunze kujenga tabia ya kutekeleza kila unachoahidi kwako na kwa wengine.
You Deserve The Best!
Vicent Stephen

UTAANZA KUFANIKIWA PALE UTAKAPOANZA KUTEKELEZA KILA AHADI UNAYOITOA
Reviewed by By News Reporter
on
8/08/2018 11:17:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: